Kadhia ya Palestina kwa mtazamo wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Kadhia ya Palestina ni mhimili wa umoja wa Waislamu wote. Mkutano wa sita wa kuunga mkono Intifadha ya Palestina ulianza asubuhi ya leo hapa mjini Tehran kwa hotuba ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ambayo ilijikita zaidi katika kubainisha masuala ya kiistratejia na ya msingi katika suala la Palestina.

Sababu ya kuendelea hujuma za kigaidi Somalia

Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa Somalia Michael Keating amelaani hujuma ya kigaidi iliyojiri Jumapili katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu huku wengi wakihoji sababu ya kuendelea hujuma za kigaidi nchini humo.

Kuendelea mgogoro Sudan Kusini na kujiuzulu maafisa kadhaa wa jeshi na serikali

Mgogoro wa kisiasa wa Sudan Kusini umepanuka zaidi hadi serikalini ambapo siku kadhaa zilizopita baadhi ya viongozi wa serikali ya nchi hiyo wamejiuzulu nyadhifa zao.

Muungano wa Uturuki, Saudia na Israel katika propaganda chafu dhidi ya Iran

Muungano na misimamo ya aina moja dhidi ya Iran ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Waziri wa Vita wa utawala ghasibu wa Israel na mwenzao wa Uturuki katika Mkutano wa Usalama wa Munich si jambo jipya wala lililotokea kwa sadfa.