Pars Today ni tovuti ya habari ya nchini Iran ambayo ilianzishwa mwezi Julai 2016 kwa kutumia uzoefu wa zaidi ya miaka 70 wa huduma za matangazo ya ng'ambo za Sauti na Televisheni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB ikiwa na muundo mpya wa kihabari. Tovuti hii ni ya kupasha habari na kuakisi matukio mbalimbali duniani kwa kutumia zaidi ya lugha 30 hai za dunia. (Lugha nyingine mpya ziko mbioni kuanzishwa).

Pars Today inatoa huduma za habari zikiwemo tovuti, redio, matangazo kupitia frikwensi, Intaneti na simu za mkononi, kama ambavyo inapatikana vizuri katika mitandao ya kijamii. Lugha za Kiswahili, Kihausa, Kiingereza, Kiarabu, Kifaransa, Kirusi, Kijerumani, Kiitaliano, Kihispania, Kireno, Kiarmenia, Kialbania, Kichina, Kijapani, Kikazaki, Kiebrania, Kiurdu, Kihindi, Kibangladeshi, Kipashtu na Kimaleyu ni miongoni mwa lugha zinazotumiwa na Pars Today.

Matukio ya kisiasa ya Mashariki ya Kati na nafasi ya Iran ikiwa ni nchi yenye taathira katika eneo hili na pia nchi yenye usalama na inayozidi kupiga hatua za kimaendeleo, ni mambo ambayo yanayoifanya Pars Today kuwa chombo cha habari chenye taathira.

Pars Today kwa lugha ya Kiswahili ni chombo cha habari chenye taathira ambacho kinazalisha habari za kisiasa, kiutamaduni na kidini na kuzirusha hewani kwa shabaha ya kufichua yasiyosemwa na vyombo vingine vya habari duniani.

Walengwa wa Pars Today kwa lugha ya Kiswahili ni mamilioni ya wazungumzaji wa lugha hiyo walioenea katika kona zote za dunia ambao wanafuatilia matukio mbalimbali yanayohusiana na Iran, Mashariki ya Kati, nchi zinazozungumza Kiswahili na maeneo mengine ulimwenguni.

 

Usiache kuwa pamoja nasi.