Sisitizo la Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu juu ya kulindwa utambulisho wa Kiislamu na maarifa ya Qur'ani

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, hii leo ulimwengu wa ukafiri umekusudia kufuta kabisa utambulisho wa Kiislamu katika kila pembe ya dunia. Ayatullah Sayyid Ali Khamenei alisema hayo jana Alkhamisi alipokutana na maustadhi, maqarii na mahufadhi wa Qur'ani Tukufu walioshiriki katika Mashindano ya 34 ya Kimataifa ya Qur'ani hapa nchini Iran kutoka nchi 83 za dunia na kubainisha kwamba, utambulisho wa Kiislamu unazuia uingiliaji na ubeberu wa maadui.

Putin asisitiza udharura wa kuwepo msimamo mmoja katika kupambana na ugaidi

Rais Vladmi Putin wa Russia amesema katika ujumbe uliosomwa kwenye Mkutano wa Sita wa Usalama wa Kimataifa mjini Moscow kwamba, mapambano dhidi ya ugaidi katika eneo la Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika yanahitaji kuwa na mtazamo na msimamo mmoja na unaooana.

Umoja wa Mataifa na udharura wa kuzingatia mustakbali wa mateka wa Kipalestina

Umoja wa Mataifa umebainisha wasiwasi wake kuhusu hali waliyonayo mateka wa Kipalestina katika jela za utawala wa Kizayuni ambao wameanzisha mgomo wa kula chakula wakitaka kuboreshewa hali zao kwenye jela hizo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atahadharisha kuhusu hali mbaya ya watu wa Yemen

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, watoto zaidi ya 50 wa Yemen wanafariki dunia kila siku kutokana na hali mbaya inayotawala nchi hiyo.

Kuanza maneva ya "Simba wa Afrika" nchini Morocco

Maneva ya kijeshi yaliyopewa jina la "Simba wa Afrika" yameanza katika nchi ya Kiafrika ya Morocco yakishirikisha askari wa Jeshi la Majini la Marekani na wanajeshi 1300 kutoka nchi nyinginen 11.

Kushadidi vitendo vya utumiaji mabavu dhidi ya Waislamu nchini Nigeria

Baada ya viongozi wa Nigeria kukataa kumuachilia huru Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, Waislamu wa nchi hiyo kwa mara nyingine tena wameandamana wakitaka kuachiliwa huru mwanaharakati huyo wa Kiislamu.

Takwa kwa jamii ya kimataifa la kuingilia haraka kadhia ya Libya

Kufuatia kuendelea vurugu na machafuko nchini Libya na kuweko uwezekano wa kuibuka tena vita vya ndani katika maeneo ya kusini mwa nchi hiyo, Serikali ya Maafikiano ya Kitaifa ya Libya imeitaka jamii ya kimataifa iingilie kati mgogoro wa nchi hiyo na kuhitimisha machafuko ya ndani.

Kulaaniwa uingiliaji wa Marekani katika masuala ya ndani ya Zambia

Sambamba na kuendelea vuta nikuvute ya kisiasa kuhusiana na uchaguzi uliopita nchini Zambia, Rais Edgar Lungu wa nchi hiyo ameashiria uingiliaji wa Marekani na Umoja wa Ulaya katika masuala ya ndani ya nchi hiyo hususan kutiwa mbaroni kiongozi wa wapinzani na kulaani vikali uingiliaji wa madola ya kigeni katika masuala ya ndani ya Zambia.