Idara ya uhamiaji nchini Kenya imepunguza mawakala wanaojihusisha na kusafirisha raia wa Kenya kwenda kufanya kazi katika mataifa ya Mashariki ya Kati kutoka 500 hadi 23 katika kile ilichokieleza kuwa ni kuleta uwajibikaji katika shughuli hizo.

Hayo yamekuja kufuatia kuongezeka vilio vya wafanyakazi hao huko ughaibuni ikiwemo kufanyiwa ukatili na kunyimwa haki zao. Kwa mujibu wa idara hiyo, kila mwezi serikali ya Kenya hutumia kiasi cha baina ya Dola elfu 40 hadi elfu 50 katika kusimamia shughuli za kuwarudisha makwao raia wa taifa hilo waliokwama katika mataifa ya ughaibuni.

Raia wa Kenya wanaofanya kazi za ndani Saudia wakilia kutokana na ukatili wanaokabiliana nao 

Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa idara ya uhamiaji nchini humo Meja Jenerali Mustaafu Gordon Kihalangwa. Kuhusiana na suala hilo, Redio Tehran imefanya mahojiano na Bi. Zamzam Muhammed, naibu mweka hazina wa kitaifa wa mwamvuli wa mawakala nchini kenya……………/

 

Apr 13, 2017 17:01 UTC
Maoni