Manusura wa mauaji ya kimbari ya Rwanda ya mwaka 1994 huko wilaya ya Karongi magharibi mwa nchi hiyo, wameyalaani majeshi ya Ufaransa kwa kuhusika kwao kwa kiwango cha juu kwenye mauaji hayo.

Viongozi wa Rwanda akiwemo Anastase Murekezi, Waziri Mkuu wa nchi hiyo kwa mara nyingine tena wameinyooshea kidole cha lawama Ufaransa kwa kujiingiza kwake moja kwa moja kwenye mauaji hayo.

Askari wa Ufaransa wakiwa pamoja na genge la vijana wa Kihutu kwenda kutekeleza mauaji ya kimbari mwaka 1994

Hayo yanajiri katika hali ambayo, licha ya kutolewa thibitisho mbalimbali juu ya namna Paris ilivyohusika katika jinai hizo, lakini hadi sasa nchi hiyo ya Ulaya imeendelea kukanusha suala hilo, na hivyo kuufanya uhusiano wa nchi mbili kuendelea kuzorota.

Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera anaripoti zaidi………../

 

 

Apr 13, 2017 17:17 UTC
Maoni