Apr 14, 2017 08:18 UTC
  • Uingereza: Machafuko ya Sudan Kusini ni sawa na mauaji ya kimbari

Waziri wa Serikali ya Uingereza amesema kuwa mauaji yaliyoyalenga makundi maalumu ya kikabila huko Sudan Kusini na kusababisha vita vya ndani nchini humo mwaka 2013, ni sawa na mauaji ya kimbari.

Priti Patel, Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Uingereza amesema baada ya kurejea nchini akitokea ziarani Sudan Kusini kuwa, ni wazi kwamba mauaji yaliyojiri nchini humo ni ya kikabila na kwa msingi huo, yanahesabiwa kuwa ni mauaji ya kimbari. Patel amesema kuwa vikosi vya jeshi la serikali ya Sudan Kusini wiki hii vimekuwa vikiyashambulia makundi mahsusi ya watu huko Wau mji wa pili kwa ukubwa nchini Sudan Kusini.

Wanajeshi wa Sudan Kusini wanaotuhumiwa kutekeleza mauaji ya kimbari 

Wakati huo huo Michael Makuei, Waziri wa Habari wa Sudan Kusini amekadhibisha matamshi ya Waziri huyo wa Uingereza akisema kuwa, ni ya upotoshaji.

Vita vya ndani vilianza Sudan Kusini mwaka 2013 kufuatia kuibuka makabiliano ya kuwania madaraka kati ya Rais Salva Kiir wa nchi hiyo kutoka kabila la Dinka na makamu wake wa zamani, Riek Machar kutoka jamii ya Nuer. 

Tags

Maoni