• Benki ya Dunia ina matumaini na ustawi wa kiuchumi Afrika

Benki ya dunia inasema kasi ya ukuaji wa uchumi barani Afrika inaridhisha mwaka huu ikilinganishwa na mwaka jana ambapo uchumi wa bara hilo uliporomoka kwa kiwango kikubwa zaidi katika kipindi cha miongo miwili.

Katika ripoti yake kuhusu hali ya uchumi barani Afrika, benki ya dunia imesema bara hilo sasa limeonyesha matumani ya ukuaji wa uchumi ambapo ulikadiriwa kufikia asilimia 2.6 mwaka huu ikiwa ni ongezeko lililopindukia ukuaji wa asilimia 1.6 wa mwaka jana.

Nchi zinazoongoza kwa kiwango cha juu cha uchumi ambazo ni Nigeria, Afrika Kusini na Angola, zilioneka kuporomoka mwaka jana na ukuaji wa uchumi katika nchi hizo ulikuwa ukisuasua kutokana na kutopungua kwa bei za bidhaa na ukosefu wa sera makini.

Huduma za fedha za simu za mkononi

Nchi za kusini mwa jangwa la Sahara zimeonekana kuchanua katika ukuaji zikiwemo Tanzania , Kenya na Rwanda huku Mali, Senegal na Kodivaa, nazo zikijitutumua .

Punam Chuhan mtaalamu wa masuala ya uchumi katika Benki ya Dunia anaseman moja ya changamoto za Afrika ni kuweza kuimarisha uwekezaji wa sekta zote ya umma na binafsi. 

Apr 21, 2017 06:42 UTC
Maoni