• Hitilafu kati ya Misri na Sudan zapamba moto zaidi

Sudan imewasilisha malalamiko yake dhidi ya Misri katika Umoja wa Mataifa kuhusu umiliki wa maeneo ya Hala'ib na Shalatiin.

Sudan leo imewasilisha rasmi malalamiko yake kwa Umoja wa Mataifa ikipinga dikrii ya Rais wa Misri kuhusu umiliki wa maeneo ya Hala'ib na Shalatiin iliyotolewa miaka 27 iliyopita.

Katika malalamiko hayo yaliyotolewa kwa kuchelewa dhidi ya Misri, Sudan imesisitiza kuwa eneo la Hala'ib ni milki yake na kwamba eneo hilo limeghusubiwa na Misri. Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Misri na Sudan jana walifanya mazungumzo kujadili umiliki wa maeneo hayo mawili ya Hala'ib na Shalatiin; mazungumzo ambayo hata hivyo hayakufikia natija. 

Maeneo ya Hala'ib na Shalatiin yanaendelea kugombaniwa na Misri na Sudan tangu nchi hizo mbili zilipopata uhuru kutoka kwa mkoloni Muingereza. Maeneo hayo yanapatikana katika mpaka wa pamoja wa nchi mbili hizo.

Eneo la Halayeb kama linavyoonekana kwenye ramani  

Itakumbukwa kuwa, wakati wa ziara iliyofanywa huko Cairo, Misri na Rais Omar Hassan al Bashir wa Sudan mwezi Oktoba mwaka 2014 na mazungumzo aliyofanya na Rais wa nchi hiyo, Abdel Fattah al Sisi, pande mbili zilikubaliana kuweka kando hitilafu zilizopo kwa maslahi ya kuimarisha ushirikiano wa nchi mbili hizo. 

Apr 21, 2017 15:56 UTC
Maoni