• Kenya: Wanamgambo 52 wa al Shabab wameuawa Somalia

Jeshi la Kenya limewauwa wanamgambo 52 wa kundi la kigaidi la al Shabab katika shambulio lililofanyika hii leo kwenye kambi ya kundi hilo kusini mwa Somalia.

Msemaji wa Vikosi vya Ulinzi vya Kenya, Kanali Joseph Owuoth  amesema kuwa tukio hilo limejiri huko Badhaadhe katika Juba ya Chini. Kanali Owuoth ameongeza kuwa, bunduki, vifaa vitatu vya milipuko na zana na kutengenezea mabomu zimenaswa katika shambulio hilo dhidi ya al Shabab.

Wanamgambo wa al Shabab, Somalia

Itafahamika kuwa Kenya ina maelfu ya wanajeshi katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) kwa shabaha ya kuwaangamiza wanamgambo wa al Shabab na kuimarisha usalama kama sehemu ya kuijenga upya Somalia baada ya miongo miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoirudisha nyuma nchi hiyo.

Apr 21, 2017 16:28 UTC
Maoni