Watalaam wa elimu barani Afrika wamekiri kwamba ukosefu wa kiwango cha ubora wa elimu barani humo kimesababisha kudorora kwa raslimali yenye uwezo wa kuinua maendeleo kwa kasi inayotakiwa.

Hii ni moja mada muhimu ambayo imekuwa ikijadiliwa kwa siku kadhaa katika kongamano la elimu mjini Kigali, Rwanda na wawakilishi kutoka vyuo vikuu barani Afrika.

Wanafunzi wa moja ya vyuo vya Afrika wakifanya mgomo kudai mikopo

Takwimu zilizotolewa zimeonyesha kwamba katika vyuo 10 vikuu bora vya kwanza duniani, ni kimoja tu kutoka barani Afrika. Vile vile hesabu za ripoti hiyo inaonyesha kwamba, kati ya vyuo vikuu 100 bora vya kwanza duniani ni vinne tu barani Afrika na vyote hivyo vinne ni vya nchini Afrika Kusini. Hata hivyo Rais Poul Kagame wa Rwanda amewataja vijana wa Afrika kuwa wenye uwezo mkubwa wa akili ikiwa wataandaliwa mazingiza bora ya kusoma.

Jiunge na mwandishi wetu wa jijini Kigali, Silvanus Karemera kwa taarifa zaidi……/

 

 

Jul 08, 2017 09:46 UTC
Maoni