Tume ya kitaifa haki za binaadamu nchini Burundi imesema kuwa, hali ya haki za binaadam imezidi kuboreka siku hadi siku nchini.

Hayo yametolewa ikiwa ni baada ya ripoti juu ya masuala ya kibinaadamu kuwasilishwa mbele ya bunge la taifa hilo hivi karibuni. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, idadi ya watu walouawa Burundi katika kipindi cha miezi sita ya mwanzo wa mwaka huu 2017, imekadiriwa kuwa ni 69 pekee, katika hali ambayo katika kipindi kama hicho mwaka jana 2016 ilikuwa ni 340.

Sehemu ya ukiukaji wa haki za binaadamu nchini Burundi, ambapo hata watoto wadogo hawasalimiki

Hata hivyo tume hiyo imeonyesha wasi wasi wake kutokana na aina mpya ya ukiukaji wa haki ndani ya taifa hilo ikiwa ni pamoja na kupindukia idadi ya watu wanaoshikiliwa katika jela, watu kutoweka katika mazingira tatanishi, unyanyasaji wa kijinsia na biashara ya watu.

Jiunge na mwandishi wetu wa jijini Bujumbura Hamida Issa kwa taarifa kamili………/

 

Jul 08, 2017 10:32 UTC
Maoni