Nchini Rwanda zimeanza kampeini za uchaguzi wa rais ambapo Rais Paul Kagame wa nchi hiyo ameonyesha kutokuwa na wasi wasi wowote na upinzani wake.

Katika ufunguzi wa kampeni hizo, Rais Kagame amewaahidi raia wa taifa hilo kwamba, anaamini kwamba ataibuka mshindi kwa kile alichosema kuwa ni uungaji mkono mkubwa wa wananchi kwa chama chake cha RPF.

Mpayimana Philippe, mpinzai wa Rais Kagame na mgombeaji binafsi 

Hii ni katika hali ambayo wapinzani wawili wa rais huyo nao wamezindua kampeni zao nchini humo kwa kuwataka wananchi wawapigie kura ili kubadili mfumo wa uongozi nchini.

Frank Habineza, mpinzani anayechuana na Rais Kagame

Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera anaripoti zaidi

 

 

Jul 14, 2017 17:04 UTC
Maoni