Chama cha Lugha na Fasihi ya Kiswahili nchini Tanzania CHALUFAKITA imeitunuku Idhaa ya Kiswahili Sauti ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zawadi maalumu ya shahada ya kutunza lugha ya Kiswahili.

Hatua hiyo imekuja kutokana na mchango mkubwa wa Redio Tehran katika kuenzi na kutumia fasihi ya lugha hiyo katika matangazo yake.

Cheti kilichotolewa kwa ajili ya Redio Tehran

Zawadi hiyo imetolewa katika kongamano la siku tatu la Kiswahili lililofanyika visiwani Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali, waandishi na wataalamu wa Kiswahili kutoka Afrika Mashariki.

Ili kujua zaidi kuhusiana na tukio hilo tumefanya mahojiano na Salma Said, mwandishi wa habari ambaye alihudhuria kongamano hilo na kwanza tumeanza kwa kumuuliza.

 

Aug 05, 2017 17:25 UTC
Maoni