Wapinzani wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameitisha mgomo wa nchi nzima dhidi ya serikali ya Rais Joseph Kabila wa nchi hiyo.

Watu 14 waliuawa kwa kupigwa risasi katika vurugu zilizotokea Jumatatu ya jana katika jiji la Kinshasa na mji wa Matadi, kusini mwa nchi hiyo.

Makundi ya waasi nchini humo

Kufuatia hali hiyo wapinzani wa serikali wameitisha mgomo wa nchi nzima leo na kesho kupinga mwenendo huo wa serikali sambamba na kuishinikiza serikali kutangaza tarehe ya uchaguzi.

Taarifa kamili  tujiunge na mwandishi wetu wa eneo la katikati mwa Afrika Mosi Mwasi....../

Aug 08, 2017 17:02 UTC
Maoni