Usalama umeimarishwa kikamilifu katika maeneo yanayoaminika kuwa ngome za upinzani nchini Kenya kwa lengo la kuzuia machafuko.

Kaimu Waziri wa Usalama nchini humo amekadhibisha habari ambazo zimekuwa zikienezwa katika mitandao ya kijamii kwamba, polisi ya Kenya imetumia nguvu kukabiliana na maandamano ya amani nchini. Fred Matiang'i ameongeza kwa kusema kuwa, polisi hawajatumia risasi halisi kukabili waandamanaji ambao kuanzia jana wamekuwa wakikabiliana na polisi mitaani huku wakipora na kuharibu mali za wananchi.

Fred Matiang'i, Kaimu Waziri wa Usalama nchini Kenya

Hii ni katika hali ambayo hali inaonekana kutengamaa katika maeneo kadhaa ya Kenya baada ya kutangazwa matokeo rasmi ya uchaguzi uliopita nchini humo.

Kwa maelezo zaidi tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Mombasa Seifullah Murtadha…………/

 

 

Aug 12, 2017 16:13 UTC
Maoni