Kwa mara ya kwanza barani Afrika kumeanzishwa jukwaa la wanasayansi wanaolenga kutatua changamoto mbalimbli za maendeleo zinazolikabili bara hilo hususan katika sekta ya kilimo.

Ni jukwaa la wanasayansi wa ngazi ya juu kwenye nyanja zote ambalo linawajumuisha wanasayansi wa Kiafrika wanaoishi na kufanyia kazi katika maeneo yote ulimwenguni.

Kilimo bora Afrika

Jukwaa hilo limeanzishwa mjini Kigali Rwanda chini ya ajenda ya kuboresha sekta ya kilimo kwa kutumia sayansi ili kuzalisha mazao mengi kinyume na kilimo cha zamani.

Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera anaripoti zaidi

 

 

Sep 07, 2017 14:33 UTC
Maoni