• Wamisri wataka wapinzani wa serikali ya Syria wafukuzwe nchini kwao

Wananchi wa Misri wameitaka serikali ya nchi hiyo kuwatimua wapinzani wa serikali ya Syria walioko nchini humo.

Wananchi wa Misri wanasema kuwa, wamedanganywa kuhusu mgogoro wa Syria na kwa msingi huo wanaharakati wa masuala ya sheria na haki za binadamu wameanzisha mchakato wa kuhakikisha kwamba, wapinzani wa serikali ya Syria wanafikuzwa nchini humo.

Sambamba na hayo Dua Saleh ambaye ni afisa wa Kamati ya Wananchi ya Mfungamano ya Watu wa Syria nchini Misri na Wakili Muhammad Abu Zaid wameweasilisha mashtaka mahakamani wakitaka kufutwa amri iliyotolewa miaka kadhaa iliyopita na aliyekuwa rais wa nchi hiyo Muhammad Morsi ya kukatwa uhusiano wa kidiplomasia baina ya Cairo na Damascus. 

Serikali ya sasa ya Misri imekuwa na msimamo unaotofautiana na sera za serikali ya kabla yake kuhusu mgogoro wa Syria na inasisitiza udharura wa kuangamizwa kundi la kigaidi la Daesh huko Syria ambalo wanachama wake pia wamekuwa wakifanya mashambulizi ya kijilipua kwa mabomu katika ardhi ya Misri hususan katika peninsula ya Sinai.    

Sep 12, 2017 14:59 UTC
Maoni