Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kwa kushirikiana na mashirika mengine 102 ya utetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania yamelaani vitendo vya uhalifu vinavyoendelea kama shambulizi la risasi kwa viongozi mbalimbali, pamoja na matukio ya utekaji nyara wa watu.

Mambo hayo yanasababisha kuibuka kwa taharuki na hofu ya kiusalama kati ya Watanzania.

Dr. Hellen Kijo Bisimba, Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania 

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini (LHRC) Dr. Hellen Kijo Bisimba, Tanzania ni nchi inayoongozwa na mfumo wa kidemokrasia na utawala bora hivyo kuendelea vitendo hivyo ni suala linaloweza kuitumbukiza nchi hiyo katika hali ya mchafukoge.

Tujiunge na mwandishi wetu wetu Silvano Kayera kutoka Dar es Salaam Tanzania kwa taarifa zaidi…......./

 

Sep 12, 2017 18:17 UTC
Maoni