• Tanzania na Kenya kufanya mazungumzo ya biashara Novemba

Kenya na Tanzania zitafanya mazungumzo mwezi Novemba ili kuimarisha biashara kati ya pande hizo mbili.

Katibu mkuu wa wizara ya viwanda, biashara na ushirikiano nchini Kenya Chris Kiptoo amesema mjini Nairobi kuwa, nchi hizo mbili zina wasiwasi baada ya kushuka kiwango  cha biashara baina yao tangu mwaka 2015.

Amesema pande mbili zimekubaliana kukutana mjini Mombasa kwa ajili ya kutafuta njia ya kuondoa vizuizi vya ushuru ambavyo vinasababisha kushuka kwa biashara.

Habari hiyo inatolewa wiki moja baada ya Kenya na Tanzania kufanya mazungumzo ya siku tatu mjini Dar es Salaam, Tanzania.

Matrela yakiwa na mizigo

Mazungumzo hayo yalilenga kutatua vizuizui vya biashara ya bidhaa kama vile maziwa, tumbako, gesi na nyama.

Kumekuwepo na mvutano wa muda mrefu wa kibiasahra kati ya Kenya na Tanzania jambo ambalo limepelekea kudhoofika jitihada za kuleta ushirikiano zaidi baina ya nchi tano za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Sep 13, 2017 07:50 UTC
Maoni