Oct 01, 2017 03:59 UTC
  • Wanajeshi vamizi wa Sudan wapata pigo, mamia wauawa nchini Yemen + Picha

Toleo la mtandaoni la gazeti la al Akhbar la nchini Lebanon limetangaza habari ya kushindwa vibaya wanajeshi vamizi wa Sudan nchini Yemen. Kwa upande wake, mtandao wa habari wa Yemen Press umeandika kuwa, zaidi ya wanajeshi 400 wa Sudan wameshauawa hadi hivi sasa huko Yemen.

Katika ripoti yake ya jana, gazeti la al Akhbar limeandika kuwa, Rais Omar al Bashir wa Sudan amekwama katika kinamasi kikubwa na hivi sasa anapoteza wanajeshi wake mmoja baada ya mwingine nchini Yemen.

Baadhi ya wanajeshi wa Sudan waliouawa nchini Yemen

 

Gazeti hilo limeongeza kuwa, pigo na maafa wanayopata wanajeshi wa Sudan ambao wameingia katika mkumbo wa kuivamia Yemen baada ya kushawishiwa na Saudia Arabia, yanaongezeka siku baada ya siku.

Toleo la mtandaoni ni la gazeti hilo limeongeza kuwa, kwa hatua yake ya kufuata mkumbo wa Saudia na Imarati, si tu kwamba Rais Omar al Bashir amewapeleka machinjioni wanajeshi wa Sudan, lakini pia hakuna manufaa yoyote ya kisiasa aliyoyapata.

Kitambulisho wa mwanajeshi wa Sudan aliyeuawa nchini Yemen

 

Utawala wa kiimla wa Saudi Arabia na baadhi ya nchi za Kiarabu waliivamia Yemen mwezi Machi 2015 kwa baraka kamili za Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel na kuizingira kila upande, angani, ardhini na baharini nchi hiyo maskini ya Kiarabu kwa tamaa kwamba wangeliwashinda nguvu kirahisi wananchi wa Yemen.

Hata hivyo hadi hivi sasa uvamizi huo wa Saudia na wenzake umeshindwa kufua dafu mbele ya muqawama wa kiume wa wananchi Waislamu wa Yemen.

Pamoja na hayo hadi hivi sasa uvamizi huo umeshapelekea zaidi ya raia 12 elfu wa Yemen kuuawa na makumi ya melfu ya wengine kujeruhiwa. Mamilioni ya raia wa Yemen wamekuwa wakimbizi na miundombinu ya nchi hiyo maskini ya Kiarabu imeharibiwa kikamilifu.

Tags

Maoni