Familia ya mbunge wa Singida mashariki na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Upinzani  nchini Tanzania  Tundu  Lissu, imelilalamikia jeshi la polisi la nchi hiyo kutokana na hatua yake ya kuchelewa katika kufanya uchunguzi wa tukio la kupigwa risasi ndugu yao.

Kwa mujibu wa wanafamilia hao, kwa kuzingatia kuwa awali Lissu alikuwa ameelezea suala la yeye kufuatiliwa na watu wasiojilikana, hivyo kufahamika kwa wahusika wa hujuma dhidi yake lingekuwa jambo lepesi.

Siku ambayo Tundu Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana

Kadhalika ndugu wa Tundu Lissu wamewataka polisi nchini humo kushirikiana na vyombo vingine vya kimataifa ili kuwabaini wahusika.

 Mwandishi wetu  Silvano Kayera kutoka Dar es salaam Tanzania anataarifa zaidi. Bonyeza juu ili kupata sauti............../

 

 

Oct 05, 2017 15:52 UTC
Maoni