Ripoti ya matukio ya Kiislamu kuanzia nchini Tanzania ambapo Waislamu wameonyesha kusikitishwa kutokana na bomoabomoa inayoendelea jijini Dar es Salaam. Hatua hiyo imekuja baada ya kuwekwa alama ya x kwenye misikiti 16 kwa ajili ya kubomolewa.

Hii ni katika hali ambayo aghlabu ya misikiti hiyo imekuwa ikitumika kwa ajili ya swala ya Ijumaa. Tukitokea Tanzania tunaelekea nchini Kenya ambapo Waislamu wa nchi hiyo wamekosoa baadhi ya misimamo ya viongozi wa kisiasa katika kufumbia macho haki muhimu za Waislamu hususan hatua yao ya kuipuuza siku ya Ijumaa ambayo Waislamu huwa wanatakiwa kwenda kushiriki swala ya Ijumaa.

Waislamu nchini Tanzania

Mbali na suala hilo pia Waislamu wa nchi hiyo wakalalamikia hatua ya kutaka kumpokonya ushindi mwanamke Mwislamu anayevaa hijabu Bi Khadija Nganyi Juma na hivyo wameitaka serikali ichukue hatua ya haraka ili kumuapisha mwanamke huyo.

Ripoti hiyo imeandaliwa na mwandishi wetu wa visiwani Zanzibar Hassan Issa Ali.....Bonyeza juu kusikiliza sauti............/

 

Oct 06, 2017 16:41 UTC
Maoni