Rais John Pombe Magufuli wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amewaapisha mawaziri na Manaibu Waziri ambao wametokana na mabadiliko madogo aliyoyafanya kwenye baraza lake la mawaziri.

Rais Magufuli alifanya mabadiliko hayo hapo tarehe  saba Oktoba mwaka huu ikulu ya jijini Dar es Salaam.

Rais Magufuli akiwa na baraza lake la Mawaziri

Katika mabadiliko hayo Magufuli aliwapiga kalamu nyekundu baadhi ya mawaziri, kuwapandisha baadhi ya manaibu na kuwa mawaziri sambamba na kuwateua makada wengine kwenye nafasi hizo.

Mwandishi wetu wa jijini Dar es Salaam Silvano Kayera ametuandalia taarifa Zaidi……Bonyeza juu kusikiliza sauti………../

 

Oct 09, 2017 16:37 UTC
Maoni