• Rwanda yatajwa kuzuia safari ya timu ya kuzuia utesaji ya Umoja wa Mataifa

Kamisheni ya Kuzuia Utesaji ya Umoja wa Mataifa imeahirisha safari ya ujumbe wa kamisheni hiyo kwenda Rwanda.

Taarifa iliyotolewa na kamisheni hiyo imesema kuwa, sababu ya kuahirishwa safari hiyo kwenda nchini Rwanda ni kuwepo vizuizi kutoka kwa viongozi wa nchi hiyo mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Kadhalika kamisheni hiyo imeelezea wasiwasi wa watu wanaohojiwa kutokana na kufuatiliwa na viongozi wa serikali ya Kigali.

Kitengo cha kamisheni hiyo kinachohusika na kuzuia utesaji ambacho kiko chini ya Umoja wa Mataifa, kilikuwepo nchini Rwanda kwa kipindi cha miaka mitano, hata hivyo mwishoni kilitangaza kuwa hakiwezi tena kutuma ujumbe wake katika nchi hiyo.

Rais Paul Kagame wa Rwanda anayenyoshewa kidole cha lawama kwa utesaji wa wapinzani

Katika ripoti hiyo imeelezwa kuwa, hii ilikuwa mara ya tatu kwa kamisheni hiyo kufanya safari nchini Rwanda. Kamisheni ya Kuzuia Utesaji ya Umoja wa Mataifa inahusika na ufuatiliaji wa hatua na vitendo vya utumiaji mabavu vya jeshi na maafisa usalama wa serikali dhidi ya wapinzani wa Rais Paul Kagame wa nchi hiyo. Wapinzani wa Rais Kagame wanamkosoa kiongozi huyo kwa kutumia jeshi katika kuwatisha wapinzani. Aidha wanaikosoa serikali ya kiongozi huyo kwa kuimarisha usalama kwa kutumia vitisho.

Tags

Oct 22, 2017 03:08 UTC
Maoni