• Zarif aonana na Rais na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda mjini Kampala + Picha

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameonana na Rais Yowezi Kaguta Museveni wa uganda mjini Kampala na pande hizo mbili zimejadiliana masuala ya pande mbili na ya kieneo na kimataifa.

Vile vile Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameonana na Sam Kutesa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda mjini Kampala na pande mbili zimesisitizia ulazima wa kuimarishwa ushirikiano wa pande mbili katika nyuga zote.

Shirika la habari la IRNA limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, mazungumzo ya Zarif na Sam Kutesa yamefanyika leo na mawaziri hao wawili wamejadiliana masuala ya pande mbili hususan ya kisiasa, kiuchumi na kibiashara.

Waziri Zarif katika mazungumzo na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Uganda, Sam Kutesa

Mambo mengine yaliyojadiliwa na mawaziri wa mambo ya nje wa Iran na Uganda mjini Kampala ni ya kieneo na kimataifa. Kabla ya hapo pande hizo mbili zilikutana katika shehere za ufunguzi wa jumuiya ya wafanyabiashara wa Iran na Uganda mjini Kampala.

Itakumbukwa kuwa sherehe za ufunguzi wa jumuiya ya wafanyabiashara wa Iran na Uganda zimefanyika pia leo Jumatano na kuhudhuriwa na ujumbe wa ngazi za juu wa nchi mbili ulioongozwa na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo.

Jana Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aliondoka Pretoria, mji mkuu wa Afrika Kusini kuelekea Kampala Uganda.

Tags

Oct 25, 2017 16:00 UTC
Maoni