•  Wanamgambo wa al Shabab zaidi ya 100 wauawa katika shambulio la Marekani Somalia

Jeshi la Marekani limeeleza kuwa limeuwa wanamgambo wa kundi la al Shabab zaidi ya 100 katika shambulio la ndege za kivita za nchi hiyo dhidi ya kambi ya kundi hilo huko Somalia.

Kamandi ya jeshi la Marekani barani Afrika (AFRICOM) imesema katika taarifa yake hapo jana kuwa shambulio hilo la anga lilifanywa umbali wa kilomita 200 kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Taarifa ya Africom imeongeza kuwa, wanajeshi wa Marekani jana walitekeleza shambulio hilo la anga dhidi ya kambi la kundi al Shabab kwa kushirikiana na vikosi vya serikali ya Somalia. Shambulio hilo lilitekelezwa muda wa sasa nne na nusu asubuhi kwa wakati wa Somalia ina kuuwa wanamgambo wa al Shabab zaidi ya 100.

wanamgambo wa kundi la al Shabab lenye makao yao Somalia 

Kumekuwa na hali ya utata kuhusu mashambulizi ya ndege za Marekani zisizo na rubani(drone) na mengine ya anga katika maeneo ya vijijini huko Somalia; nchi ambayo ingali inajikongoja kutoka katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu vya zaidi ya miongo miwili. Duru za ndani nchini Somalia zinasema kuwa mashambulizi kama hayo pia yamekuwa yakisababisha vifo vya raia wa kawaida.

 

 

Tags

Nov 22, 2017 03:05 UTC
Maoni