Kwa mara ya kwanza katika historia ya Uislamu nchini Burundi kumezinduliwa tafsiri ya Qur'ani nzima kwa lugha ya Kirundi.

Mkuu wa kamati iliyoendesha kazi hiyo amesema, haikuwa kazi rahisi kwani walikutana na pingamizi za kila namna. Kazi hiyo ilichukuwa muda wa miaka minane kukamilika. Mwandishi wetu Hamisa Issa ana malezo zaidi kutoka jijini Bujumbura.

Tags

Dec 26, 2017 09:40 UTC
Maoni