Tanzania ndio nchi ambayo imeonekana kuwa na kiwango kikubwa cha ukuaji uchumi katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo kwa mwaka huu uchumi wake umekuwa kwa asilimia 6.8 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu.

Katika hatua nyingine Waziri wa Fedha wa Tanzania Philp Mpango amesisitiza kwa mara nyingine indhari ya Rais John Pombe Magufuli ya wale waotoa takwimu zilizo kinyume na zile za serikali na kuahidi kuwachukulia hatua kali wale waliohusika na utoaji wa takwimu hizo mbali na zile za serikali.

Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Dar es Salaam Silvano Kayera kwa taarifa kamili……/

 

Tags

Dec 29, 2017 17:06 UTC
Maoni