Rais Yoweri Museveni wa Uganda ametia saini na kuufanya kuwa sheria muswada wa kuondoa kikomo cha umri wa rais wa nchi hiyo, suala ambalo limemfungulia njia ya kuwania tena urais mwaka 2021.

Sheria ya awali ilikuwa inamzuia mgombea kuwania urais baada ya kufikia umri wa miaka 75. Kwa mujibu wa sheria hiyo ya awali, Museveni ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 73 asingeliruhusiwa kuwania tena urais katika uchaguzi ujao.

Tarehe 10 Disemba 2017, bunge la Uganda lilipasisha muswada wa kuondoa kizuizi hicho cha umri kwa wingi wa thuluthi mbili ya wabunge waliohudhuria kikao hicho.

Iwapo Museveni atashinda katika uchaguzi wa 2021 ataweza kuendelea kuwa rais wa Uganda hadi mwaka 2031.

Tags

Jan 03, 2018 07:34 UTC
Maoni