Jan 13, 2018 18:49 UTC

Huku dunia ikiendelea kulaani vikalai matamshi ya Rais Donald Trump wa Marekanmi aliyoyatoa siku ya Alkhamisi iliyopita ambapo aliyashambulia mataifa ya bara hilo na kuyafananisha na shimo la choo, Waafrika wameenonyesha kuchukizwa na kitendo huku wengine wakitaka kuchukuliwa hatua kali dhidi ya rais huyo.

Katika uwanja huo baadhi ya Wafrika wamezitaka nchi za Afrika kuwatimua mabalozi wa Marekani sambamba na kuwarejesha nyumbani mabalozi wao walioko Marekani ili kuionyesha Washington thamani ya bara hilo.

Bendera za kupendeza za nchi za bara la Afrika

Kadhalika wengine wamemtaka rais huyo kujiangalia mwenyewe kama anayo hadhi ya kulingana thamani ya Afrika.

Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Dar es Salaam Tanzania Omar Manji kwa taarifa kamili........./

 

Tags

Maoni