• Polisi Kenya yamkamata mbunge wa tatu aliyeshiriki hafla ya kujiapisha Odinga

Polisi ya Kenya imemtia nguvuni kwa muda na kumsaili mbunge wa tatu wa kambi ya upinzani nchini humo kwa tuhuma ya kushiriki katika hafla ya kuapishwa kinara wa kambi ya upinzani Raila Odinga kuwa "kiongozi wa wananchi" badala ya Rais Uhuru Kenyatta wa nchi hiyo aliyeshinda uchaguzi wa Oktoba mwaka jana.

George Aladwa ambaye ni mbunge wa chama cha National Resistance Movement cha Odinga amekamatwa na polisi mjini Nairobi na kusailiwa kuhusiana na kuapishwa kwa kinara wa NASA. Aladwa ambaye amekanusha kufanya kosa lolote, ametakiwa kuripoti tena polisi siku ya Jumanne ijayo.

Kukamatwa huko kwa George Aladwa kunafuatia kule kwa mwanasiasa mwingine wa upinzani, Miguna Miguna, aliyetiwa nguvuni katika shambulizi lililofanyika alfajiri nyumbani kwake mjini Nairobi siku ya Ijumaa na vilevile siku moja baada ya kukamatwa kiongozi mwingine wa upinzani.

Wafuasi wa kambi ya upinzani Kenya, Bustani ya Uhuru, Nairobi

Miguna ameachiwa huru kwa dhamana na shilingi elfu hamsini.  

Serikali ya Kenya imefunga matangazo wa stesheni za televisheni za NTV, Citizen na KTN baada ya vyombo hivyo vya habari kutangaza moja kwa moja hafla ya kuapishwa kiishara kinara wa muungano wa upinzani wa NASA, Raila Odinga kuwa 'rais wa wananchi' siku ya Jumanne.

Hata hivyo Mahakama Kuu ya nchi hiyo imeiamuru serikali kuruhu matangazo ya stesheni hizo za televisheni.

Tags

Feb 03, 2018 15:46 UTC
Maoni