Chama cha wananchi CUF nchina Tanzania kimekosoa matamshi ya Waziri wa Sheria wa nchi hiyo, Palamagamba Kabudi bungeni mjini Dodoma aliyesema kwamba, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayo mamlaka kuingilia masuala ya ndani ya Zanzibar hata yasiyohusuu muungano.

Mwanasheria wa chama cha Wananchi CUF na aliyewahi kuwa waziri katika serikali ya awamu ya sita visiwani Zanzibar, Abubakar Khamis Bakary sambamba na kushangazwa na kauli hiyo, amemtaka Kabudi akasome vizuri katiba ya Tanzania.

Image Caption

Ameongeza kwamba, Rais wa Jamhuri ya Muungano ana mamlaka ndani ya Zanzibar yanayohusu tu muungano na si vinginevyo.

Tujiunge na mwandishi wetu wa visiwani Zanzibar Harith Subeth kwa taarifa kamili……………/

 

 

 

Tags

Feb 08, 2018 15:37 UTC
Maoni