Nchini Burundi, leo kumezinduliwa zoezi la uorodheshaji wa majina ya wapiga kura katika daftari la kudumu kuelekea kura ya maoni hapo baadaye.

Kwa mujibu wa Gaston Sindimwo Makamu wa Kwanza wa Rais wa nchi hiyo, watakaojiandika katika daftari la kudumu safari hii, watapata fursa ya kushiriki katika kura ya maoni ambayo itafanyika mwaka 2020, kwa lengo la kumpa nafasi Rais Pierre Nkurunziza aendelee kusalia madarakani Zaidi.

Gaston Sindimwo Makamu wa Kwanza wa Rais wa nchi hiyo

Hata hivyo katika siku ya kwanza ya zoezi hilo, kulikuwa na idadi ndogo ya watu waliofika katika vituo vya kujiandisha.

Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Bujumbura Hamisa Isa kwa taarifa kamili………./

 

Tags

Feb 08, 2018 15:40 UTC
Maoni