• UN: Mashambulizi dhidi ya wanamgambo DRC yatawalazimisha maelfu ya raia kuyahama makazi yao

Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuwa, mashambulizi yanayoendelea dhidi ya wanamgambo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo huwenda yakawalazimisha raia wapatao 370,000 kuyahama makazi yao.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu imesema katika ripoti yake ya jana kuwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wasiopungua laki mbili kuna uwezekano wakayahama makazi yao katika mkoa wa Beni na wengine 170,000 katika eneo jirani la Lubero kutokana na oparesheni  zinazofanywa na jeshi la serikali dhidi ya wanamgambo katika mikoa ya Kongo karibu na mpaka na Uganda.

Vikosi vya jeshi la Kongo katika oparesheni dhidi ya wanamgambo 

Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa, hadi sasa raia wa Kongo wasiopungua milioni 4.3 wamekuwa wakimbizi kutokana na kuendelea mapigano dhidi ya uasi wa makundi ya wanamgambo katikati mwa nchi hiyo na pia kufuatia kushtadi mzozo katika maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo katika mipaka na Uganda, Rwanda na Burundi.  

Umoja wa Mataifa umelitaja tatizo hilo la wakimbizi kuwa ni tatizo kubwa barani Afrika.

Tags

Feb 09, 2018 07:10 UTC
Maoni