• Hujuma ya kigaidi msikitini Benghazi, Libya, watu kadhaa wauawa au kujeruhiwa

Watu kadhaa wanaripotiwa kupoteza maisha au kujeruhiwa katika mji wa Benghazi nchini Libya kufuatia hujuma ya kigadi wakati wa Sala ya Ijumaa hii leo.

Baadhi ya taarifa zinasema  mfuko uliokuwa na mabomu ndnai yake ulilipuka karibu na mlango wa msikiti katika eneo la Majuri na kupelekea watu wanane kupoteza maisha na wengine karibu 40 kujeruhiwa.

Hadi sasa hakuna kundi lililodai kuhusika na hujuma hiyo ya kigaidi. Pamoja na hayo kuna taarifia za kutatanisha kuhusu tukio hilo huku baadhi ya ripoti zikisema ni milipuko miwili iliyojiri na kwamba ni mtu moja tu ndiye aliyeuawa.

Mwezi ulipoita watu wasiopungua 33 waliuawa na wengine wapatao 50 kujeruhiwa baada ya magari mawili yaliyotegwa mabomu kuripuka katika mji wa Benghazi ulioko mashariki mwa Libya. Mwezi huo huo takriban watu 27 walipoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa karibu na msikiti mmoja katika mji huo huo wa Benghazi kufuatia hujuma ya kigaidi.

Jenerali Khalifa Haftar

Benghazi ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Libya baada ya mji mkuu wa nchi hiyo, Tripoli. Mji huo ambao ulikuwa kituo kikuu cha mapinduzi ya mwaka 2011 na makao makuu ya wanamapinduzi waliomuondoa madarakani Kanali Muammar Gaddafi, umekuwa katika ghasia na machafuko makubwa yaliyoanza mwaka 2014 hadi mwishoni mwa mwaka jana. Nukta ya kuashiriwa kuhusu Benghazi ni kuwa, tofauti na miji mingine ya Libya kama Tripoli, Tobruk na Al Baida ambayo inatawaliwa na serikali kadhaa kwa wakati mmoja, mji huo haujawahi kudhibitiwa na serikali yoyote ile kati ya serikali zinazodhibiti maeneo mbalimbali ya Libya. Mji huo zaidi unadhibitiwa na makundi ya wanamgambo na waasi wenye silaha huku Jenerali Khalifa Haftari akiwa kiongozi wa mji huo.

Tags

Feb 09, 2018 15:18 UTC
Maoni