Serikali ya Rwanda imeanza zoezi la kufanya sensa ya kuwaorodhesha wakimbizi wote wanaoishi nchi hiyo.

Rwanda imesema kwamba, inafanya hivyo kwa lengo la kutambua idadi kamili ya wakimbizi hao ili kurahisisha katika kuwapatia huduma bora, na kuhakikisha usalama wao.

Wakimbizi wakiwa nchini Rwanda katika mazingira magumu

Inakadiriwa kwamba hadi sasa Rwanda ina jumla ya wakimbizi laki moja na elfo 70 kutoka Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambao waliingia nchi hiyo kutokana na machafuko ndani ya nchi zao.

Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylivanus Karemera anaripoti zaidi…………./

Tags

Feb 11, 2018 07:54 UTC
Maoni