Taharuki imetanda visiwani Zanzibar baada ya kukithiri matukio ya kutoweka katika mazingira ya kutatanisha, wanaharakati wa taasisi za Kiislamu katika visiwa hivyo vya Unguja na Pemba.

Vyombo vya usalama hata hivyo vimejitenga na tuhuma za kuhusika na vitendo hivyo. Hatua hiyo imekuja baada ya kutoweka mlezi wa taasisi za Kiislamu Sheikh Hajj Khamis Hajj siku chache zilizopita.

Baadhi ya viongozi wa Kiislamu Zanzibar wanaoshikiliwa kwa miaka kadhaa huko Tanzania bara

Matukio ya kutoweka watu katika mazingira ya kutatanisha yamekuwa yakishuhudiwa nchini Tanzania, huku vyama vya upinzani vikiitaja serikali kuhusika na matukio hayo.

Baadhi ya bendera za vyama vya upinzani

Hii ni katika hali ambayo hadi sasa masheikh kadhaa wa Kiislamu visiwani humo bado wanaendelea kushikiliwa katika korokoro za serikali Tanzania bara kwa miaka kadhaa sasa bila kufunguliwa mashitaka.

Mwandishi wetu wa Zanzibar, Harith Subeit ana maelezo zaidi......./

 

Tags

Feb 13, 2018 07:41 UTC
Maoni