• Mbunge wa Tunisia achana bendera ya Israel ndani ya Bunge

Mbunge mmoja wa Tunisia amechana bendera ya utawala wa Kizayuni wa Israel, kuonyesha ghadhabu zake dhidi ya serikali ya nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika ya kutaka kufanya wa kawaida uhusiano wake na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Ammar Amroussia, mbunge wa upinzani alipasua bendera ya Israel katika kikao cha jana Bungeni, akishinikiza kuwasilishwa na kujadiliwa muswada kuhusu uhusiano wa Tel Aviv na Tunis.

Hivi karibuni, jumuiya ya waungaji mkono wa Palestina nchini Tunisia ikiongozwa na muungano wa mrengo wa kushoto wa upinzani, iliwasilisha muswada katika Bunge la nchi hiyo unaolitaka likihesabu kuwa ni uhalifu kitendo chochote cha kujaribu kuwa na uhusiano wa kawaida na Israel.

Tunisia kama nyingi za Kiarabu, haina uhusiano wa kidiplomasia na utawala haramu wa Israel.

Watunisia katika maandamano ya kuiunga mkono Gaza, Palestina

Mwishoni mwa mwaka uliopita, wananchi wa Tunisia walifanya maandamano mbele ya bunge la nchi hiyo wakilitaka lipasishe sheria ya kulihesabu suala la kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa ni uhalifu.

Waandamanji hao aidha walitoa nara za kuunga mkono Palestina na kutangaza upinzani wao kwa uamuzi wa hivi karibuni wa rais wa Marekani Donald Trump aliyeitambua rasmi Quds kuwa eti ni mji mkuu wa utawala wa Kizayuni. 

Tags

Feb 14, 2018 07:22 UTC
Maoni