• Kituo cha polisi chashambuliwa Afrika Kusini, polisi wauawa

Watu waliokuwa na silaha wameshambulia kituo cha polisi katika mji mdogo wa Nqcobo nchini Aftrika Kusini na kuua polisi wasiopungua 5 na mwanajeshi mmoja.

Polisi ya Afrika Kusini imetangaza kuwa, askari polisi na mwanajeshi huyo wameuawa leo wakati waliposhambuliwa na kundi la watu waliokuwa na silaha katika kituo hicho cha polisi.

Msemaji wa Polisi ya Afrika Kusini, Brigedia Vishnu Naidoo amesema kuwa shambulizi hilo limefanyika mapema leo katika mji wa Nqcobo ulioko umbali wa yapata kilomita 800 kutoka Johannesburg.

Ameongeza kuwa watu hao wanaoshukuliwa kuwa ni majambazi walifyatua risasi ovyo na kuiba silaha na gari moja la polisi.

Uhalifu umekithiri Afrika Kusini

Waziri wa Polisi wa Afrika Kusini, Fikile Mbalula amelitaja shambulizi hilo kuwa ni janga la kitaifa. 

Afrika Kusini inahesabiwa kuwa miongoni mwa nchi zenye viwango vya juu zaidi vya uhalifu duniani.   

Tags

Feb 21, 2018 14:28 UTC
Maoni