Mwangwi wa hatua ya Rais Yoweri Kaguda Museveni wa Uganda ya kumtimua Inspekta Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini humo Jenerali Kale Kayehura na maafisa wengine kadhaa wa masuala ya usalama umeendelea kuhisika huku wananchi wakitoa maoni mbalimbali kuhusu hatua hiyo.

Aliyeshuka nafasi hiyo hivi sasa ni Jenerali Okoth Ochola aliyekuwa naibu wa Jenerali Kale Kayihura. Kwa upande wake, gazeti la Daily Monitor la Uganda limeripoti habari ya kukabidhiwa Jenerali Kayihura kwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC kujibu mashtaka mbalimbali ya uhalifu. 

Mwandishi wa Radio Tehran Idhaa ya Kiswahili nchini Uganda, Kigozi Ismail ametuandalia ripoti maalumu kuhusu suala hilo.

Inspekta Jenerali wa Polisi wa zamani wa Uganda, Kale Kayihura

 

Tags

Mar 06, 2018 07:18 UTC
Maoni