Wazanzibar wameonyesha kuvutiwa na Msyria kwa jina la Twariq Muhammad Samir al-Abad ambaye baada ya kukimbia vita nchini kwao alielekea visiwani humo kwa ajili ya kuendeleza maisha yake.

Hayo yamedhihiri baada ya raia huyo wa Syria kufungua mgahawa ambao amekuwa akipika vyakula mbalimbali maarufu katika eneo la Mashariki ya Kati. Kwa upande wake Samir al-Abad mbali na kufurahishwa na mazingira ya Zanzibara, ametaka pia kupewa uraia ili amalizie sehemu iliyobakia ya maisha yake nchini Tanzania.

Mgahawa wa Damascus Kitchen uliofunguliwa na Twariq Muhammad Samir al-Abad huko ZNZ

Mgogoro wa Syria ulianza mwaka 2011, baada ya magaidi wa Kiwahabi kuanzia Daesh (ISIS), Jab'hatu Nusra na mfano wa hayo na chini ya uungaji mkono kamili wa Marekani, Uingereza, Ufaransa, Israel, Saudia, Imarat na baadhi ya nchi, kuanzisha hujuma za kila upande kwa lengo la kutaka kuiondoa madarakani serikali halali ya Rais Bashar al-Assad, ili kwa njia hiyo yaweze kudhamini usalama utawala haramu wa Israel. Hata hivyo njama hizo zimefeli kutokana na kusimama imara jeshi la Syria kwa kushirikiana na harakati ya Hizbullah ya Lebanon, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pamoja na Russia dhidi ya njama hizo chafu.

Bonyeza alama ya sauti ili uweze kujiunga na mwandishi wetu wa visiwani Zanzibar Harith Subeit kwa taarifa kamili……………/

 

Tags

Mar 07, 2018 16:28 UTC
Maoni