• Maelfu ya wakimbizi wa Burundi wahamia Rwanda kutoka Congo DR

Wakimbizi elfu mbili na mia tano wa Burundi wameingia katika nchi ya Rwanda wakitokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Idara ya Kutoa Huduma kwa Wakimbizi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza kuwa, wakimbizi wa Burundi waliokuwa katika kambi ya wakimbizi ya Kamanyola katika mkoa wa Kivu Kusini kwa sasa wamevuka mpaka na kuingia Rwanda. 

Msemaji wa timu ya kusimamia amani ya Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Florence Marshall ameashiria maombi ya wakimbizi wa Burundi ya kusaidiwa kuondoka katika kambi ya Kamanyola na kuingia Rwanda na kusema kuwa, idara ya timu hiyo pia imewasaidia wakimbizi hao kwa mujibu wa majukumu yake. 

Wakimbizi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Florence Marshall amesema kuwa, wakimbizi hao wa Burundi wameamua kuhamia Rwanda kwa kuhofia operesheni ya maafisa wa serikali ya Congo ya kurejeshwa kwa nguvu nchini kwao. 

Kuwepo kwa wakimbizi wa Burundi huko mashariki mwa Congo kumesababisha machafuko na mivutano ya mara kwa mara baina ya maafisa wa serikali na wakazi wa maeneo hayo. Burundi inataka wakimbizi hao warejeshwe nchini humo.  

Tags

Mar 08, 2018 08:18 UTC
Maoni