Mei 21, 2018 14:00 UTC
  • Jeshi la Libya latangaza kulitia mbaroni kundi linalomuunga mkono Kanali Muammar Gaddafi

Kundi lenye mafungamano na Baraza la Kuu la Serikali ya Maridhiano ya Kitaifa nchini Libya, limetangaza kuwatia mbaroni wanachama wanaouunga mkono utawala wa Kanali Muammar Gaddafi, kiongozi wa zamani wa nchi hiyo.

Al-Rad'u al-Khaswimah, lenye mafungamano na Baraza Kuu la Maridhiano ya Kitaifa nchini Libya limetoa taarifa likisema kuwa, genge hilo linalojiita 'Mrengo wa Wananchi kwa ajili ya Ukombozi wa Libya' linaongozwa na Saif al-Islam Gaddafi, mtoto wa Kanali Muammar Gaddafi. Taarifa hiyo imeeleza kwamba kundi hilo ambalo linaungwa mkono na mrengo wa Kitaifa wa Uhuru nchini Libya, linaongozwa na idara ya operesheni kusini mwa Tripol, mji mkuu wa Libya kwa lengo la kuendesha harakati zake ndani ya mji huo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na al-Rad'u al-Khaswimah, watu waliotiwa mbaroni wamekiri kuhusika na vitendo vya uharibifu katika miji tofauti ya Libya kama ambavyo pia wamenaswa na silaha na zana mbalimbali za kijeshi, magari na ramani za kijeshi katika maficho yao. Kundi la Mrengo wa Wananchi kwa ajili ya Ukombozi wa Libya ambalo linaundwa na waungaji mkono wa Kanali Muammar Gaddafi, lilitangaza uwepo wake tarehe 26 Disemba mwaka 2016.

Tags

Maoni