Mei 24, 2018 07:36 UTC
  • Tahadhari yatolewa kuhusu hatari ya kujipenyeza zaidi Wazayuni barani Afrika

Waziri wa zamani wa masuala ya kidini wa Senegal ametahadharisha kuhusu hatari ya kuzidi kujipenyeza Wazayuni barani Afrika.

Mtandao wa Intaneti wa Bawabat Afriqiyyah umemnukuu Mammado Bumba Anjie, waziri wa zamani wa masuala ya kidini wa Senegal akitoa tahadhari hiyo na kusisitiza kuwa, fikra za walio wengi huko Senegal zimezingirwa na Wazayuni na wafuasi wa utawala huo ghasibu.

Amesema, pamoja na hivyo bado ana imani na wananchi Waislamu la Senegal kwamba watasimama imara kukabiliana na wakanushaji Mungu na waeneza fitna wote.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akiwekeana saini mkataba na Benjami Netanyahu, waziri mkuu wa utawala dhalimu wa Israel

 

Waziri huyo wa zamani wa Senegal amezungumzia namna idadi ya wafuasi wa utawala wa Kizayuni inavyoongezeka barani Afrika na kusema kuwa, hatari hiyo imelikumba bara la Afrika kutokana na nchi za Kiislamu na Kiarabu kushindwa kutekeleza wajibu wao barani humo.

Amesema hivi sasa Togo imekuwa kama mwakilishi wa utawala wa Kizayuni wa Israel huko magharibi mwa Afrika kiasi kwamba hivi karibuni ilifanya juhudi za kuitisha kikao cha Israel na Afrika ingawa hata hivyo imekwamishwa na mazingira ya kisiasa ya barani humo.

Kabla ya hapo pia baadhi ya waandishi wa habari na wabunge wa nchi za Kiarabu barani Afrika kama vile Tunisia waliwahi kuonya kuhusu hatari ya kujipenyeza Wazayuni barani humo.

Tags

Maoni