Mei 25, 2018 03:19 UTC
  • Al Azhar yalaani kitendo cha balozi wa Marekani cha kuufuta msikiti wa Al Aqsa katika taswira ya Quds

Chuo Kikuu cha kidini nchini Misri cha Al Azhar kimelaani hatua ya balozi wa Marekani Israel David Friedman ya kuonyesha picha ya mandhari ya mji wa Baitul Muqaddas isiyo na msikiti mtukufu wa Al Aqsa ndani yake.

Al Azhar imetoa taarifa ya kulaani kitendo cha Friedman cha kuonyesha picha ya mji wa Baitul Muqaddas (Jerusalem) ambao ndani yake, badala ya msikiti mtukufu wa Al Aqsa, unaonekana mchoro wa hekalu bandia linalodaiwa na wazayuni kupasa kuwepo katika eneo hilo.

Taarifa hiyo ya Al Azhar imesisitiza kuwa hatua hiyo haramu na ya kinyume cha sheria haitoweza kuibadilisha historia na kwamba Quds itaendelea kubaki kuwa mji mkuu wa nchi ya Palestina.

Taswira potofu na bandia ya mji wa Baitul Muqaddas

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo imetahadharisha kuwa kimya kinachoonyeshwa kwa hatua za ukiukaji sheria zinazoendelea kuchukuliwa na mhimili wa Kizayuni na Kimarekani, kinaitia hatarini amani na usalama wa eneo la Mashariki ya Kati.

Siku ya Jumanne ya tarehe 22 Mei, ilichapishwa picha inayomuonyesha balozi wa Marekani Israel David Friedman akiwa ameshika mkononi mwake taswira bandia ya wazayuni ya ujenzi wa hekalu la Kiyahudi kwenye eneo lenye magofu ya msikiti mtukufu wa Al Aqsa, kibla cha kwanza cha Waislamu.

Kitendo hicho kimetonesha hisia za kidini na kuamsha hasira za Waislamu wa Palestina.../

Tags

Maoni