Mei 25, 2018 15:27 UTC

Wakati Afrika ikiadhimisha siku ya 'Ukombozi wa Bara la Afrika' watafiti na wasomi mbalimbali wamekosoa utumiaji mabavu wa watawala wa nchi za bara hilo dhidi ya wananchi wanaowakosoa kutokana na uongozi wao mbovu serikalini.

Kadhalika wamekosoa uingiliaji kati wa mataifa makubwa katika utendajikazi wa bara hilo. Taarifa iliyowasilishwa na wasomi hao katika kikao kilichofanyika mjini Kigali, Rwanda imesema kuwa uingiliaji huo wa madola ya kigeni umesababisha kudhoofika kwa juhudi za maendeleo barani Afrika.

Waafrika wakiwa na matumaini ya kufikia demokrasia lakini imekuwa ndoto isiyofikiwa

Aidha wamelaumu viongozi wa mataifa ya Afrika kwa kuendekeza ukandamizaji dhidi ya raia wao ilhali walitakiwa kuwafariji na kuwatumikia.

Kutoka Kigali mwandishi wetu Sylvanus Karemera anaripoti zaidi……./

 

 

 

Tags

Maoni