Jun 28, 2018 15:49 UTC

Viongozi wa upinzani nchini Tanzania wameendelea kukosoa bajeti ya serikali yam waka wa fedha 2018-2019 wakidai kuwa bajeti hiyo si rafiki wa wananchi.

Hayo yamekuja ikiwa ni baada ya kupitishwa bajeti hiyo kwa kishindo hivi karibuni mjini Dodoma na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa mujibu wa viongozi hao wa upinzani, bajeti hiyo haijazingatia hata kidogo maslahi ya wafanyakazi, wabuvi, wakulima sambamba na kuwasahau pia wastaafu.

Philip Mpango, Waziri wa Fedha wa Tanzania

Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini na Mwenyekiti taifa wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania  cha Demokrasia na Maendelea (CHADEMA), Freeman Mbowe, wamesema kuwa bajeti hiyo imeshushwa kwa asilimi 23 katika sekta ya kilimo ambayo wananchi walio wengi wanapata kipato chao.

Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Dar es Salaam kwa taarifa kamili……………../

 

Tags

Maoni