Jul 07, 2018 17:04 UTC

Sakata la kuwekwa kodi kwa mitandao ya kijamii nchini limezidi kutokota ambapo mara hii kundi la wanaharakati kwa kushirikiana na viongozi wa upinzani wameitisha maandamano ya nchi nzima kupinga kodi hiyo.

Wanaharakati hao wamesema kuwa, kodi hiyo haijazingatia uhalisia wa maisha ya Waganda na hivyo wameitaja kuwa itakayo athiri sehemu kubwa ya raia wa nchi hiyo. Hii ni katika hali ambayo matumizi ya utumaji na upokeaji fedha kwa njia za simu nayo yamesimama kufuatia kupanda kodi ya huduma hiyo.

Sakata la mitandao ya kijamii nchini Uganda

Aidha wakati Rais Museven ametaka kodi hiyo ishushwe kwa asilimia 50, mamlaka husika zilikuwa zimekusudia kupandisha kodi hiyo kwa kiwango zaidi, huku wapinzani wao wakitaka ifutwe kabisa.

Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Kampala, Kigozi Ismail kwa taarifa kamili……Bonyeza juu kupata sauti……./

 

Tags

Maoni