Jul 12, 2018 07:35 UTC
  • Ethiopia: Kufunguliwa tena barabara zinazoelekea katika bahari Nyekundu ni kipaumbele

Ethiopia imesema kuwa inataka kulipa kipaumbele suala la kuzifungua tena barabara mbili zinazoiunganisha nchi hiyo na bandari mbili za Eritrea zilizopo katika bahari Nyekundu kufuatia kufikiwa mapatano baina ya nchi mbili hizo.

Nchi mbili hizo jirani za Pembe ya Afrika Jumatatu iliyopita zilikubaliana kufungua balozi zao, kuendeleza shughuli za bandari na kuanzisha tena safari za ndege kati ya pande mbili baada ya nchi mbili hizo kufikia mapatano yaliyohitimisha mzozo wa miaka 20 baina ya nchi hizo jirani. Weledi wa mambo wanasema kuwa mapatano hayo ya kihistoria huenda yakapelekea kutekelezwa mageuzi ya kisiasa na kiusalama katika eneo la Pembe ya Afrika lililokumbwa na maachafuko.

Ahmed Shide msemaji wa serikali ya Ethiopia amesema kuwa kufunguliwa tena kwa barabara hizo muhimu zinazoelekea katika bandari za Assab kusini mwa Eritrea na huko Massawa kaskazini mwa nchi hiyo kutakuwa kwa manufaa ya eneo zima.

Aidha jana Jumatano Waziri Mkuu wa Ethiopia Ahmad Abiy aliandika katika mtandao wake wa kijamii wa twitter kwamba raia wa Ethiopia na Eritrea wenye hati za kusafiria wanaweza kufanya safari katika nchi mbili hizo na kupewa viza baada ya kuwasili.

Ahmed Abiy, Waziri Mkuu wa Ethiopia 

Tags

Maoni