Jul 12, 2018 15:57 UTC

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Demokrasia na Maendelea (CHADEMA) kimeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kusimamia kwa haki uchaguzi mdogo wa ubunge na udiwani katika eneo la Buyugu mkoani Kigoma.

Kwa mujibu wa viongozi wa chama hicho, iwapo tume hiyo haitosimamia vyema zoezi hilo, huwenda kukaibuka ghasia na machafuko. Kadhalika wamesisitiza kwamba, kuzingatiwa kanuni na sheria za uchaguzi, huleta maelewano na utulivu katika kila nchi.

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendelea (CHADEMA) Tanznaia, Vincent Mashinji

Uchaguzi mdogo katika eneo la Buyugu umepangwa kufanyika tarehe 12 Agosti mwaka huu.

Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Dar es Salaam Amari Dachi kwa taarifa kamili.

 

Tags

Maoni